Uchambuzi wa Zaburi 22, 23 na 24

UTANGULIZI

Wakati Yesu amefufuka na habari zake zikizidi kuenea, kuna tukio moja ambalo Daktari Luka anaandika kwenye ile Luka 24. Maandiko yanasema,

Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha. Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe” – Mstari wa 13 mpaka wa 27

Angalia maneno ya Yesu mwenyewe anaposema, Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!. Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?” (Mstari wa 25 na 26)na baadaye maandiko yanasema Yesu alianza kutoa shule, Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe” (Mstari wa 27)

Kitu gani cha kujifunza hapa,

  • Maisha na huduma ya Yesu vilishatabiriwa kabla na kilichotabiriwa na manabii kilibeba ujumbe huu, Yesu ni mwokozi, mchungaji na mfalme wetu mkuu.
  • Miongoni mwa waliotabiri kuja kwa Yesu, maisha yake na huduma yake ni Musa, Daudi, Isaya na wengine wengi. Kwa mfano, Musa kwenye Kumbukumbu la Torati 18:15 “Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru”

Kama ilivyokuwa kwa Nabii Yona kukaa ndani ya tumbo la samaki kwa siku tatu, ilikuwa ni unabii kumhusu Yesu atakavyokaa katika moyo wa nchi. Maandiko yanasema, Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi” – Mathayo 12:39

Sasa, hata kwa mtumishi wa Mungu Daudi, katika Zaburi hizi tatu, ya 22, 23 na 24 kupitia mapito yake binafsi alitabiri habari za Yesu katika maeneo matatu, yaani Yesu kama mwokozi, mchungaji na mfalme.

Zaburi ya 22 inaonesha kuja kwa Yesu mara ya kwanza kama mwanakondoo wa Mungu ambaye alijitoa mwenyewe kama dhabihu kwa ajili yetu, juu ya Kalvari. Kwa kifupi, Zaburi hii inamfunua Yesu kama mwokozi

Zaburi ya 23 inaonesha huduma ya Yesu ya wakati huu kama mchungaji mkuu mwema wa kondoo. Kama mchungaji mwema anatujali, anatuongoza, anatulea, anatulinda na anatuombea.

Zaburi ya 24 inamwonesha Yesu kama mfalme wetu mwenye utukufu mwingi ambaye atarudi kutawala dunia katika haki na amani ya kweli.

Sasa tuchambue kwa undani zaidi

Somo litaendelea

Leave a comment