‭‭1 Sam‬ ‭30:6‬ ‭SUV‬‬

[6] Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini *Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake*.

Maisha yetu yamejawa na changamoto za aina mbalimbali na kila mmoja hupitia kwa nafasi yake na hatuwezi kufanana.

Jambo la kujiuliza,

huwa ni kipi ambacho tuna kifanya kwanza katika tunayoyapitia na Je ni njia gani hutumika kutatua au kutafuta suluhisho.

Katika kila tunalokutana nalo lililo gumu yatupata kujitia Nguvu katika Bwana .

Kujitia Nguvu katika Bwana ni hali ya kumtumaini Mungu na kutegemea msaada kutoka kwake katika lile unalolipitia.

Lolote linalo kuja kwako Mungu analosuluhisho na anaweza kutuletea msaada na kutufanya kuvuka na kushinda.

‭‭Zab‬ ‭121:1‭-‬2‬ ‭SUV‬‬

[1] Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? [2] Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.

Mwimba Zaburi, alikuwa katika changamoto na akaona hakuna tumaini au msaada kwingine isipokuwa kwa Mungu pekee.

Hata mimi na wewe pamoja na utashi na uwezo ambao tunao BADO tunahitaji msaada wa Mungu katika kuvuka yale tunayokutana nayo

Unapo weka tumaini na kutegemea msaada wa Bwana MUNGU huachilia nguvu ndani yako.

Nguvu unayopokea toka kwa Bwana inakufanya uweze kushinda au kukuvusha katika lile unalolipitia.

Ufanye nini ili kujitia nguvu katika Bwana?

1. Mtegemee Mungu na tegemea msaada wake.

‭‭Zab‬ ‭56:3‭-‬4‬ ‭SUV‬‬

[3] Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe; [4] Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini?

[11] Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

Pamoja na ukubwa au uzito wa changamoto,usiondoe tumaini lako katika Bwana .

Siku ya hofu yako Mtumaini Bwana pekee.

2. Usiache kumsifu Mungu.

Katikati ya changamoto yako jifunze kumsifu Mungu na usiwe mwepesi wa kulalamika.

‭‭Zab‬ ‭59:16‭-‬17‬ ‭SUV‬‬

[16] Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio *siku ya shida yangu*. [17] Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu.

3. Endelea kuomba

usiache kumwita Bwana katika lile linalokukabili.

‭‭Zab‬ ‭62:1‭-‬2‬ ‭SUV‬‬

[1] Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, Wokovu wangu hutoka kwake. [2] Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana.

Endelea kumngoja Bwana ukiwa katika hali ya maombi.

4. Nafsi yako iambatane na Bwana.

Pamoja hilo jaribu au changamoto, nafsi yako iambate na BWANA maana ndiye nguvu zako na msaada wako.

Usikubali kujitenga na Bwana sababu ya hilo lilokupata.

‭‭Zab‬ ‭63:8‬ ‭SUV‬‬

[8] Nafsi yangu inakuandama sana; Mkono wako wa kuume unanitegemeza.

‭‭Zab‬ ‭63:1‬ ‭SUV‬‬

[1] Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.

Mungu ni mwaminifu ukimtafuta anapatika

Somo limeandaliwa na Mchungaji Samweli Mmasi – 0620 390 866/0766 870 922

3 thoughts on “KUJITIA NGUVU KATIKA BWANA

Leave a comment