2. Unapopita katika magumu, tembea katika njia za Mungu (usiache ibada)

Kwenye mapito magumu unaweza kujikuta njia panda, ukimbie ibada au uendelee na ibada.

Kukimbia ibada inakusogeza karibu na kusanyiko la watenda mabaya, watu waovu, wanafiki na wenye ubatili. Ukichagua upande huu huwezi kupata upenyo kwenye mapito magumu

Daudi anatufundisha upande wa kuchagua, kuendelea na ibada, kutembea katika njia za Mungu hata wakati wa magumu kwani siri ya kushinda ipo kwenye kutokuacha ibada. Angalia maneno ya Daudi

…nimekwenda katika kweli yako. Sikuketi pamoja na watu wa ubatili, Wala sitaingia mnamo wanafiki. Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu. nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako. Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi Bwana” – Mstari wa 3, 4 – 5, 8 na 12

Jambo la kujifunza hapa ni kwamba, usitangetange, ila kusanyika kwenye kanisa la kiroho ambalo panasisitizwa utakatifu na kukatazwa maisha ya dhambi

3. Unapopita katika magumu, jitie nguvu katika Bwana na kuhitaji msaada wake.

Kujitia nguvu katika Bwana ni kujipa moyo na kuamua kumtegemea Mungu. Daudi aliigundua siri hii na ndiyo maana anasema, Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini” – Zaburi 27:3

Tukijenga tabia ya kuutafuta uso wa Bwana, tunakuwa wepesi wa kumtegemea Mungu.

Uliposema, Nitafuteni uso wangu, Moyo wangu umekuambia, Bwana, uso wako nitautafuta” – Zaburi 27:8

HITIMISHO

Ukipita kwenye mapito magumu shauku yako huwa ni nini?

Shauku ya Daudi ilikuwa, Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake” – Zaburi 27:4

Tukiwa na shauku ya aina hii tutapiga hatua toka eneo la kukata tamaa hadi eneo la imani kwa Mungu wetu.

MWISHO.

Somo limeandaliwa na Daudi Lubeleje

UNAJUA KWAMBA HUU NDIO WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI YA

KUMPOKEA YESU?

Photo by Muhammad-taha Ibrahim on Pexels.com

Claude Monet’s Madame Monet and Her Son (1875).
Original from the National Gallery of Art. Digitally enhanced by rawpixel.

Leave a comment